Kila ifikapo tarehe 1/12 ya kila mwaka dunia nzima huazimisha Siku ya Ukimwi Duniani. Ni siku inayotumiwa na wanaharakati na wakuu wa nchi, kutoa elimu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi, kupiga vita unyanyapaa na kuhimiza watu kwenda kufanya vipimo ili kufahamu hali zao.
Maadhimisho haya yamekuwa yakiadhimishwa tangu mwaka 1988, lengo kubwa likiwa ni kutoa elimu kuhusu namna ya kuepuka ugonjwa huu.
Woga, unyanyapaa na kupuuza ni mambo ambayo yanaendelea kuitesa dunia katika mapambano ya ugonjwa huu ambao umesababisha vifo vya Mamilioni ya watu tangu miaka 1980.
Maambukizi mapya yanawaathiri idadi kubwa ya vijana walio na umri wa kati ya miaka 15-25. Katika vijana watano, watatu ni vijana wa kike.
Ili kupunguza maambukizi kwa vijana, watalaam wanapendekeza kuwa, wasichana wapate nafasi ya kwenda shuleni kwa wingi, uzuiaji wa dhuluma dhidi ya wanawake lakini pia kuongezeka kwa huduma ili kutolewa kwa elimu ya afya ya uzazi.
Mtu anaweza kupata vipi HIV ?
- Kushiriki ngono na mtu aliyeambukizwa bila kutumia kinga.
- Kutumia sindanio au kitu chenye ncha kali kilichotumiwa na mtu aiyeambukizwa, hasa wale wanaojidunga dawa za kulevya.
- Kutoka kwa mama, kwenda kwa mtoto hasa kwa kumyonyesha. Mama mwenye HIV hastahili kumyonyesha mtoto.
- Kuingiziwa damu, iliyoambukizwa virusi vya HIV.
Kujikinga na HIV
- Kutumia kinga, mpira wa Condom
- Kuepuka ngono, hasa kwa vijana hadi kuoa au kulewa
- Ukiolewa kuwa mwaminifu kwa mwezi wako.
UKIMWI UPO NA UNAUA, PIMA AFYA YAKO LEO