MUFTI WA ZANZIBAR AWAONGOZA VIONGOZI WA DINI KUPATA CHANJO YA UVIKO 19

Viongozi wa dini mbalimbali nchini leo wamechanja chanjo ya Uviko 19 aina ya Johnson Johnson ili kujikinga na maradhi hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mnazimmoja mara baada yakumaliza zoezi la chanjo hiyo Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi amesema kuwa wameaamua kufanya hivyo ili kuitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya kuwataka wananchi kujikinga na ugonjwa huo.

Amewataka waislamu kufuata wito wa kupata chanjo ya kuzuwia na kuepuka maambukizo kwa watu wenmgine ili kupata taifa lenye afya bora ambalo litaweza kuleta maendeleo nchini.

Aidha Mufti huyo amewasisitiza waislamu kujitokeza kwa wingi kwani chamjo hiyo ni  hiari ni vyema jamii ikashajihika kuchanja ili kudhibiti maambukizi mapya yanayoweza kujitokeza.

 Katibu wa Mufti Khalid Ali Mfaume na Naibu Kadhi wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali  wamesema kuwa chanjo aina ya Jansonjanson imethibika kitaifa na kimataifa ambayo inajulikana  nchi nyingi hasa Saudi Arabia kwa waislamu wanatarajia kufanya ibada ya Hija na Umra duniani kote.

“Mbali yakuwa chanjo hiyo ni hiari kwa waislamu ila pasitokee mmoja wapo kumuambukiza mwenziwe hivyo wamewasisitiza wananchi kufuata utaratibu wa kupata chanjo hiyo kwani kinga ni bora kuliko tiba” walifahamisha viongzi hao.

Nae Father Paropea wa Kanisa la kitope Fr, Anselmo Mwang’amba ameishukuru Serikali kwa kuwapatia chanjo hiyo na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari zaidi ili kujikinga  na uviko 19.

Loading