Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akiwa katika Ziara ya kutembelea Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja (kushoto) Daktari dhamana wa Hospitali hiyo Tamim Hamad Said.
WAZIRI wa Afya Hamadi Rashid Mohammed amesema amefurahishwa na ujenzi unaoendelea huko katika Hospital ya Kivunge katika jengo la mama na mtoto .
Hayo ameyasema huko Hospital ya Kivunge wakati alipokuwa akifanya ziara ya jengo hilo ambalo linatarajiwa kumalizika ifikapo January mwakani.
Amesema malengo ya ziara ni kuangaliya jinsi ujenzi unavyoendelea na hatua iliyofikia ikiwa ni miongoni mwa miradi ya maendeleo inayosimamiwa na Serikali ya Mapinduzi.
Aidha amesema Serikali itahakikisha jengo litakapokwisha na kufunguliwa vifaa vyote vya huduma ya mama na mtoto viweze kukamilika na kuanza huduma hizo mara moja.
“Jengo hili likimalizika liwe na vifaa vyote ili likifunguliwa huduma zianze mara moja”, alisema Waziri huyo.
Wakati huo huo Waziri Hamad alitembelea Hospitali ya Cotage ya kivunge na kujionea changamoto zinazoikabili ikiwemo upungufu wa baadhi ya vifaa vya uchunguzi na upungufu wa madaktari.
Vile vile ameahidi katika ziara yake hiyo atazifanyiya ufumbuzi changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo ili huduma ziendelee kutolewa kwa wananchi.
Aidha sehemu alizozitembelea ni pamoja na wadi ya wazazi, sehemu ya kuhifadhia dawa na kuwasikiliza shida zao wananchi.
Nao wananchi wameishukuru Wizara ya Afya pamoja na Serikali ya Mapinduziya Zanzibar kwa kuwahudumia vyema wakati wot wanapohitaji huduma katika hospital hiyo.

Nae Mkandarasi Edwin Shittindi wa Kampuni ya WCEC Limited inayoshughulikia jengo hilo amesema ujenzi unaendelea vizuri mbali na changamoto wanazokumbana nazo .
Amesema changamoto hizo ni pamoja na mchanga ambao ulikuwa ukipatikana kwa shida na kuishukuru Wizara ya Afya na kushirikiyana na Wizara ya Kilimo kwa kuwapatia kibali na kupatikana huduma hiyo kwa urahisi.
Jengo hilo linalotarajiwa kumalizika kwake January mwakani limegharimu zaidi ya Bilioni 3 na Milioni mia tatu.