NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZINDUA JUMUIYA YA KUKUZA NA KUENDELEZA AFYA YA KINYWA NA MENO (ZOHEDO)

Naibu Waziri Wizara ya Afya  Mhe.Hassan Khamis Hafidh akizungumza na wataalamu wa Afya ya  kinywa na meno wakati akizindua rasmi  Jumuiya ya kukuza na kuendeleza Afya ya kinywa na meno Zanzibar Oral Health Development Organization (ZOHEDO) huko Ukumbi wa ZSSF Kariakooo Mjini Unguja.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Hassan Khamis Hafidh ameitaka Jumuiya ya kukuza na kuendeleza afya ya kinywa na meno Zanzibar Oral Health Development Organization(ZOHEDO)kufanyakazikwa bidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Ameyasema hayo katika Ukumbi wa ZSSF Kariakoo wakati alipokua akizindua jumuiya hiyo na kuitaka iendane na vitendo kwa kuhakikisha inaenda sambamba na kauli mbiu isemayo jivunie uzuri wa kinywa chako kwani ndio haiba na ustawi wa afya yako.

Amesema iwapo jumuiya hiyo itafanya kazi kwa pamoja na kujituma itafikia malengo waliokusudia kwani itaweza kuiasidia jamii kuibua matatizo yanayowakabili kiafya hasa katika tiba ya kinywa na meno.

Aidha Naibu Waziri amefahamisha kuwa katika sekta ya afya kuna baadhi ya watendaji hawawajibiki ipasavyo kwa kisingizio cha maslahi madogo jambo ambalo linarejesha nyuma malengo ya Serikali ya kuinua sekta hiyo ,hivyo lazima watimize wajibu wao ili kuleta mafanikio nchini.

Hata hivyo amewataka wanajumuiya hiyo kujiendeleza kielimu kwani taasisi hiyo ni yakitaalamu Zaidi.

Nae Mkuu wa Afya ya tiba yakinywa na meno Dkt Semeni Shaaban ameiomba Serikali kuwapatia ajira vijana waliomaliza stashahada zao pamoja na kupatiwa eneo lenye vitendea kazi vya kisasa ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi kwani jengo wanalotumia kwa sasa ni la kuazimwa.

Aidha amefahamisha kuwa ili jumuiya hiyo iweze kuwa mashirikiano mazuri na Wizara na jumuiya nyengine ni lazima kuwepo na mwakilishi ambae ataiwakilisha Jumuiya na kufanya kazi kwa uzuri Zaidi ili kuleta maendeleo ya afya nchini.

Kwa Upande wake Mwakilishi wa Bodi ya Udhamini katika (ZOHEDO) Dk Muhidin mesema kuwa lengo la kuwepo jumuiya hiyo ni kukuza na kuendeleza afya ya kinywa na meno na kutoa huduma bora kwajamii.

Amesema kuwa afya ya kinywa na meno ni muhimu sana na inapaswa kupewa kipaumbele zaidi kwani ipo haja yakuendelezwa kielimu vijana waliohitimu fani hiyo kwa ajili ya kuleta mafanikio.

Aidha amewataka vijana hao kufanya kazi kwajuhudi na maarifa Zaidi kwa lengo la kuisadia jamii  nje na ndani ya nchi kwani binadamu sio majaribio.

“mwanadamu anahitaji afya bora, nzuri na yenye uhakika kutokana na kusaidia kulinda afya ya mgojwa anaehitaji kutibiwa, hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa bidi na weledi mkubwa ili kuokoa afya ya wananchi kwani binadamu sio myama wala hahitaji majaribio anahitaji huduma ya uhakika”,alisema dkt Muhidin

Akisoma risala kwa niaba ya jumuiya hiyo Dk Fatma Issa amesema kuwa Jumuiya inakabili wanaukosefu wa Ofisi ya kufanyia kazi ,wafadhili pamoja na ukosefu wa mwakilishi wa daktari wa kinywa na meno katika Wizara.

Aidha amefahamisha kuwa jumuiya hiyo ni umoja ulioanzishwa kati ya wanafunzi na madaktari wote wa tiba ya kinywa na meno na kufanya tafiti nyingi nje na ndani ya Zanzibar ili kupeana habari.

Loading