ZIARA YA KUKAGUA HUDUMA ZA AFYA UWANJA WA NDEGE

 Afisa Dhamana huduma za afya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Nassor Hamadi Saidi akitowa maelezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Idara ya kinga na Elimu ya Afya, kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinisia na Watoto,  Dk. Salim Slim katika ziara ya kukagua huduma za afya Uwanja wa Ndege Zanzibar. Afisa […]

MAKABIDHIANO YA MADAWA NA VIFAA TIBA YAFANYIKA ZANZIBAR

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto (kulia)akipokea Msaada wa Madawa kutoka kwa Muakilishi wa shirika la GLOBAL LIFE SHARING Hyeksu Kim (kushoto)katika hafla ya makabidhiano iliofanyika katika Ukumbi wa Bohari kuu ya Madawa Maruhubi Zanzibar. Wizara ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa vifaa tiba na dawa mbalimbali kutoka Shirika la Global […]

MKURUGENZI TIBA WIZARA YA AFYA AZINDUA MRADI WA KUIONGEZEA THAMANI TIBA ASILI

Mkurugenzi Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar Dkt. Mayasa Salim Ali akizungumza machache na kuwakaribisha wajumbe katika uzinduzi wa mradi wa kuongezea thamani tiba asili, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mkutano Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) imetakiwa kuendeleza kufanya utafiti wa dawa za asili ili zitumike kwa usahihi katika […]

WAZIRI MAZRUI AKUTANA NA JUMUIYA YA UCHUNGUZI WA VINASABA VYA BINAADAMU TANZANIA

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itashirikiana Jumuiya ya Uchunguzi wa Vinasaba vya Binaadamu ili kugundua maradhi yanayotokana na vinasaba hivyo ili kuyapatia ufumbuzi. Ameyasema hayo Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui huko Ofisini kwake Mnazi Mmoja, wakati alipotembelewa na Ujumbe kutoka katika Jumuiya ya Vinasaba vya Binaadamu Tanzania, […]

Loading