SHIRIKA LA AFYA DUNIANI(WHO)WATAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUFANIKISHA HUDUMA ZA AFYA ZANZIBAR

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na wawakilishi  kutoka  Shirika la Afya Duniani (WHO)  wakati walipofika ofisini kwake Mnazimmoja

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema litaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar katika kufanikisha huduma za afya nchini .

Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi mkaazi  wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Nchini Tanzania Dkt. Tigest Katsele Mangestu  wakati alipokuja kumuaga  Waziri wa Afya Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui Ofisini kwake Mnazi mmoja, baada ya kumaliza muda wake wa kuitumikia nafasi hiyo

Alisema Shirika hilo litaendelea kuisaidia Zanzibar katika masuala mbali mbali ikiwemo huduma za afya kwa jamii pamoja na kuendelea na Mpango Mkakati  wa kutokomeza Kipindupindu

 Dkt. Tigest aliishukuru Serikali  kwa mashirikiano aliyoyapata wakati wa utumishi wake wa kuwakilisha Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania na kuahidi kuunga mkono katika kuleta maendeleo kwenye sekta hiyo .

Nae Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amempongeza Mwakilishi huyo kwa mashirikiano na  juhudi kubwa alizofanya za kuisaidia na kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya nchini

Amesema Shirika hilo limeweza kuwapatia taaluma wafanyakazi wa wizara ya afya na kusaidia kupunguza kuenea maradhi ya mripuko pamoja na kutoa vifaa tiba wakati wa magonjwa mbalimbali.

Waziri Mazrui ameliomba shirika hilo kuyashajihisha mashirika mengine kuja kukiendeleza kitengo cha maradhi ya mripuko ili kiweze kuimarika na kutoa huduma bora.

Katika hatua nyengne Wizara ya Afya imepokea Vifaa tiba kutoka kwa rais wa tasisi ya machozi ya furaha (Tears of joy) Jaffar Babu kwa ajili ya kusaidia huduma za Afya Nchini.

Loading