WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAPOKEA MSAADA WA DAWA KUTOKA KWA SERIKALI YA WATU WA CHINA

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed
Mazrui ameahidi kudumisha ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China ili kuinua Uchumi wa
Nchi.

Akizungumza na Balozi Mdogo wa China aliopo Zanzibar na ujumbe wake,
wakati akipokea msaada wa Dawa kutoka Serikali ya Jamuhuri ya watu wa
China Mh. Mazroui alisema Serikali hizi mbili ni marafiki wa muda mrefu
hivyo wataendeleza ushrikiano huo ili kuwapatia wananchi huduma bora za
afya.

Aidha amesema Serikali ya Zanzibar inaishukuru Serikali ya Jamuhuri ya
watu wa China kwa kushirikiana nao kwa kila hali pamoja na kuwapatia
misaada mbali mbali ikiwemo Dawa, Madaktari na Chanjo ya UVIKO-19.

“Tunishukuru Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China wamekuwa
wakishirikiana na sisi kwa kila hali hususani Wizara ya Afya kwa
kutupatia madaktari kila mwaka na misaada mbali mbali ambayo husaidia
katika kutoa huduma kwa wananchi” alisema Waziri.

Mapema Waziri Mazrui alifafanua kuwa Wizara yake imepokea Dawa 165 zenye
thamani ya takribani Shilingi Milioni 120 kwa Unguja ambazo ni idadi
sawa na Dawa zilizotolewa Kisiwani Pemba.

Kwa upande wake Balozi Mdogo wa China aliopo Zanzibar Zhan Zhisheng
amesema Serikali ya watu wa China inaahidi kuendelea kuisaidia Zanzibar
kwani tayari wameshajaza mkataba wa kujenga nyumba za wafanyakazi katika
Hospitali ya Abdalla Mzee iliopo Mkoani Pemba.

Hata hivyo Balozi Zhan amefurahishwa na mashirikiano yaliyopo baina ya
madaktari wa Zanzaibar na madaktari kutoka China katika utendaji wa kazi
unaopelekea kubadilishana Ujuzi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Makabidhiano hayo ya Dawa baina ya Wizara ya Afya Zanzibar na Serikali
ya Jamuhuri ya Watu wa China yalifanyika katika Ukumbi wa mikutano
Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed

Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.

Loading