WAZIRI MAZRUI ATEMBELEA KMKM

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na watendaji wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (hawamo pichani) mara alipofika hospitalini hapo  kuwatembelea,kushoto ni Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) Komodo Azani Hassan Msingiri.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui ameahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu na kikosi cha KMKM katika sekta ya Afya ili kutoa huduma bora kwa jamii.

Alitoa ahadi hiyo wakati alipotembelea hospital ya KMKM Kibweni Mjini Zanzibar.

Amesema kutokana na umuhimu wa Hospital ya kikosi cha KMKM ipo haja ya kufanya jitihada za kuipandisha hospital hiyo daraja kwa mujibu wa taratibu zizopangwa na kuwa Hospital ya Mkoa.

Alisema kuwa jithada za kikosi cha KMKM za kuwekeza katika miradi mbalimbali katika awamu hii ya nane, ikiwemo sekta ya uvuvi na afya ni jambo zuri ambalo litasaidia kuleta maendeleo nchini.

Aidha alikitaka Kikosi cha KMKM kutokurudi nyuma katika kufikia malengo walijiwekea, kwani dhamira yao ya kutaka kuleta maendeleo katika nchi ni jambo linalosisitizwa na Rais wa Zanzibar.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha KMKM Komodoo Azana Hassan Msingiri amesema uamuzi wa Waziri kutaka kuzitatua changamoto za hospitali ya KMKM  kwani asilimia kubwa ya huduma  zinazotolewa kwa raia wa kawaida.

Vile vile amemuomba Waziri wa Afya kuiongezea dawa hospitali hiyo ili jamii inufaike na huduma inayotolewa.

Akitaja matarajio ya hospital hiyo Daktari Mkuu wa hospital ya KMKM Mwashamba Mbarouk amesema miongoni mwa matarajio yao ni pamoja na kuongeza idadi ya madaktari, vifaa tiba na dawa ili kutoa huduma bora kwa jamii.

Alieleza kuwa Kikosi hicho kimejipanga kuanzisha bohari kuu ambayo itauza dawa kwa jumla na reja reja katika kisiwa cha Unguja na Pemba.

Loading