WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UINGEREZA ANESHUHULIKIA AFRIKA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MWERA WILAYA YA KATI UNGUJA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika  James Duddridge  amesema ataendelea kushirikiana na   Wizara ya afya Zanzibar katika kuhakikisha huduma bora za afya zinaendelea  kuimarika  nchini.

Akizungumza katika ziara yake alipotembelea kituo cha afya Mwera, Wilaya ya kati Unguja, kuona huduma zinazotolewa hasa kwa upande wa afya ya Mama na Mtoto.

Katika ziara hiyo ambayo pia ililenga kuona jinsi gani misaada mbalimbali ya afya inayotolewa na nchi yake imeweza kuwasaidia wananchi wa Zanzibar kupitia washirika mbalimbali ikiwemo mradi wa huduma za afya ya uzazi kwa wanawake, wananume,vijana,walemavu na waathirika wa ukatili wa jinsia pamoja na shirika linaloshughulikia watoto ili kuweka ustawi mzuri wa jamii Zanzibar.

Waziri James alieleza kuridhishwa na huduma zinazotolewa na wafanyakazi wa kituo cha afya cha mwera  hasa elimu ya uzazi wa mpango ambao tayari umeanza kufahamika vizuri na wanajamii pamoja na  mikakati ya kusaidia watoto ambayo imesaidia katika kupunguza mimba za utotoni nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika amewapongeza wafanya kazi wa afya pamoja na wadau wengine kwa kufanya kazi nzuri katika kuhakikisha ustawi mzuri wa jamii unapatikana hasa kupitia  uzazi wa mpango na uimarishwaji afya ya mama na mtoto.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Waziri wa Afya,Ustawi wa jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar  Nassor Ahmed Mazrui  amesema ziara ya Waziri huyo  inafaida  kubwa katika sekta afya kwani ameahidi  kuisaidia Zanzibar katika sekta ya afya ikiwemo  taaluma.

Amesema kuwa  huduma bora  zinazotolewa kituoni hapo zimemhamasisha Waziri  James na ameahidi kuendelea kutoa msaada zaidi hasa katika suala la afya ya mama na mototo pamoja na wajawazito ambao wanahitaji huduma na uangalizi zaidi wa kiafya.

“Nchi ya Uingereza imekuwa na msaada mkubwa kupitia washirika wake katika sekta ya afya Zanzibar imetusaidia kuwapatia wafanyakazi ambayo yamewawezesha  kutoa huduma bora kwa kina mama wengi na kuokoa maisha yao katika vituo mbalimbali vya afya Zanzibar ” alisema Waziri.

Akizungumzia kuhusu mimba za utotoni amesema kuwa tatizo hilo bado lipo ijapokuwa limepungua kwa asilimia kubwa tofauti na miaka iliyopita kutokana na jitahada mabalimbali za kutoa mafunzo katika maeneo ya Mjini na Vijini.

 Aidha amewapongeza viongozi wa dini kwa kusaidia serikali katika jiihada za  kutoa elimu kuhusu madhara ya mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vya mara kwa mara  kwa watoto wakati wakujifungua.

Pia Waziri Mazrui amesema bado serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana katika kituo cha afya Mwera pamoja na vituo vingine Unguja na Pemba.

Ziara hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja,Mkuu wa Wilaya Kati Unguja pamoja na wadau mbalimbali wa afya ikiwemo shirika la kushughulikia watoto duniani.

Loading