WAZIRI WA AFYA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MDOGO WA CHINA

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui ameahidi kudumisha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kukuza uchumi wa Nchi.

Akizungumza na Balozi Mdogo wa China aliopo Zanzibar huko Ofisini kwake Mnazi mmoja amesema Serikali ya China na Serikali ya Zanzibar ni marafiki wa muda mrefu hivyo wataendelea kushirikiana kwa kuwapatia huduma za afya na kukuza uchumi.

Aidha amesema Serikali ya Zanzibar imeahidi kushirikiana na Serikali ya China kuendeleza ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika Hospital ya Abdalla Mzee iliopo Mkoani Pemba ambazo zilisita kwa janga la Corona.

“Mradi wa nyumba za Wafanyakazi katika Hospitali ya Abdalla Mzee ambao Mkandarasi alishindwa kufanya kazi kutokana na Janga la Corona hivyo kwa mwaka huu wa fedha mradi wa nyumba hizo utaanza rasmin” alisema Waziri.

Nae Balozi Mdogo wa China aliopo Zanzibar Zhan Zhisheng amesema kutokana na ushirikiano huo wamekusudia kujenga Hospitali mbili za kisasa kwa Unguja na Pemba ambazo zitasidia kupunguza wimbi la wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja.  

Aidha Balozi huyo amefurahishwa na madaktari wa Zanzibar wanavyoishi vizuri na timu yas madaktari kutoka China hivyo wameahidi kudumisha urafiki baina ya nchi hizo mbili.

Loading