Waziri wa Afya , Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, akimkabidhi zawadi ya Kitabu chenye historia ya Zanzibar ndani yake Balozi wa Norway Elisabeth Jacobsen, wakati alipokuja Kumtembelea Waziri huyo Wizarani kwake Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar, na kumuahidi kuletawatafiti kutoka Norway kufanya Utafiti katika masuala ya Afya za dawa na Miti shamba
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itathamini misaada mbalimbali inayotolewa na Serikali ya Norway hasa katika nyanja ya afya na ustawi wa jamii.
Hayo ameyasema Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui huko Ofisini kwake Mnazimmoja wakati akizungumza na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Elisabeth Jacobsen.
Amesema Serikali ya Norway inaingiza fedha nyingi katika miradi ya kimataifa ambazo zinasaidia katika nyanja mbalimbali ambayo inasaidia wazee, wanawake na watoto .
Aidha Waziri Mazrui amemuomba Balozi wa Norway kuipatia Zanzibar Mashime ya kuangalia Saratani ya matiti kwa Wanawake ambayo maradhi hayo yanaathiri sana .
Nae Balozi wa Norway Nchini Tanzania Elisabeth Jacobsen amesema Serikali yake itaendelea kutoa misaada kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hasa kuchukua tahadhari ya wazee na wanawake.
Aidha amesema Serikali yake itateta watafiti ili kuona kwamba wazanzibar wanafanya tafiti za afya na matumizi ya dawa za miti shamba.