WAZIRI WA AFYA AZINDUA PROGRAMU YA JAMII NI AFYA ZANZIBAR

WAZIRI wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui amesema kuwa kuanzishwa kwa programu ya Jamii ni Afya itasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma za afya kwa urahisi.

Akizindua programu ya Jamii ni Afya kwa wahudumu wa Afya wakujitolea CHV huko Hotel Verde Waziri huyo alisema mpango huo utaisaidia jamii kutambua hatari za mapema zilizopo hasa kwa mama na mtoto pamoja kukabiliana na magonjwa mengine.

Amesema Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto itahakikisha kuwa mpango huo unawafikia watu wote na hakuna anaewachwa nyuma katika kupata huduma za Afya.
Amefahamisha kuwa taarifa zinaonyesha kuwa kuna wahudumua wa afya wa kujitolea wapatao 2300 CHV na wanasimamiwa na wasimamizi 200 kutoka vituo vya afya.

Alisema Hadi sasa takribani watu 1,300,000 wameshasajiliwa katika mfumo huu, na sasa inatoa fursa kuanza kutembelewa na kupewa elimu inayostahiki na asilimia 50 ya Watoto walioko chini ya miaka miatano na asilimia 50 ya wajawazito walifikiwa na mpango huo.

Amefahamisha kuwa program yetu ya Jamii ni Afya ni ya kipekee kwa kuwa iko katika Wilaya zote za Zanzibar na INATUMIA DIGIGITAL HEALTH. Digital Health inawasaidia CHV kufikisha ujumbe unaostahiki, kwa mtu anaestahiki na kwa wakati unaostahiki.

Ametoa wito kwa jamii kuwapa mashirikiano watoa huduma hao kwa vile wanatambuliwa na wizara ya afya na Serikali kwa ujumla.

Kwa upande wa Shirika la Unicef wamesema ni Fursa kubwa kwa nchi ya Zanzibar kuwa na Idadi kubwa ya wahudumu wa afya wa kujitolea ambao wanaifikia jamii moja kwa moja katika kuwapatia huduma za afya

Nae mwakishi kutoka d.tree Dkt Izac Hamuli amesema mpango wa progaramu ya Afya unasaidia katika kupunguza vifo vitonavyo na uzazi pamoja na kutambua change moto za afya mapema na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Kwa upande wa Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt Ali Said Nyanga Amesema kutokana na matatizo kadhaa na mahitaji ya wananchi imesababisha kuanzishwa kwa program hiyo ambayo imetoa matokeo mazuri ikiwemo kupanda kwa idadi ya kinamama wanaojifungulia vituo vya Afya

Loading