Mkutano wa Kitaalamu wa Kisayansi wa kujadili maradhi mbali mbali ya kina Mama

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inajivunia kuwepo kwa madaktari wa kichina katika kusaidia matibabu ya magonjwa mbalimbali.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Dkt Abdallah Ali Suleiman kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui huko Hospitali ya Mnazi Mmoja wakati akifungua Mkutano wa kibingwa unaohusu magonjwa ya uzazi na kinamama.

Amesema uwepo wa Madaktari wa Kichina Zanzibar kumesaidia matibabu mbalimbali ambapo hapo zamani imebidi kusafirisha wagonjwa kwenda nchi za jirani kutibiwa.

Aidha amesema Madaktari hao wa kichina kumewezesha kuwasaidia kujenga uwezo mzuri kwa Madaktari wazalendo  kufundisha mbinu za njia halisi za kisasa zenye mafanikio makubwa ya matibabu.

Dkt Abdallah amesema kwa upande wa kina mama  Hospitali ya Mnazi Mmoja imeweza kufanya Upasuaji  mkubwa kunusuru maisha kwa wagonjwa walokua hatua za kwanza za saratani ya kizazi kwa kufanyiwa upasuaji ili kusaidia kurefusha maisha.

Nae Daktari Bigwa  wa Maradhi ya kinamama na Uzazi kutoka China Xiaoqing Yang amesema lengo la Mkutano huo ni kujadiliana na Madaktari wa Hospitali ya Mnazi Mmoja na ya  Abdala Mzee maradhi yanayowasumbua akina Mama wa Zanzibar na wakichina.

Aidha amesema Mkutano huo utasaidia sana kufikisha malengo yaliyokusudiwa ili kuondosha kabisa Chngamoto zinazowakabili wakinamama wakati wa kujifungua.

Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa na Timu ya 31 ya  Madaktari Bigwa wa Kichina wa Maradhi ya Kinamama.

Loading