Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ugonjwa wa Corona na kuepuka mikusanyiko. Kuanzia leo tarehe 13/4/2020 mikutano ya waandishi wa habari na shuhuli nyengine zitakazowafanya waandishi wa habari kukusanyika zinasitishwa.

Hivyo basi, taarifa za Waziri wa Afya Zanzibar kuhusina na ugonjwa wa virusi vya Corona zitatolewa kwa njia ya “Press Release” kurusha moja kwa moja kupitia shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC) au kurekodiwa na kusambaza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari na umma kwa ujumla.

Taasisi zote zenye shuhuli zitakazowajumuisha waandishi wa habari tunawaomba kutumia njia tulizozieleza na kujiepusha kwa namna yoyote ile kuwaita waandishi wa habari katika shuhuli zao.

Waandishi na wahariri wa habari tunawasisitiza kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya na Serikali kwa ujumla kuepuka mikusanyiko.

NB: Imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zanzibar.

Loading