TAARIFA YA MWENENDO WA UGONJWA WA CORONA (COVID-19) NCHINI

Wizara ya Afya Tanzania, inatoa taarifa kuwa kati ya sampuli zilizopimwa katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii jana tarehe 16 Aprili, 2020 na leo Aprili 17, 2020 zinaonyesha kuwepo kwa wagonjwa wapya 53 wenye maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) nchini. 

Wagonjwa hawa wote ni watanzania ambao wameripotiwa katika mikoa ya Dar es Salaam (38), Kilimanjaro (1), Mwanza (1), Pwani (1), Lindi (1) na Kagera (1) wakati wagonjwa (10) wameripotiwa kuwepo Zanzibar. Aidha, tunasikitika kutangaza kifo cha mtu mmoja (1) kilichotokana na ugonjwa wa Corona nchini.  

Hivyo hadi sasa kuna jumla ya watu 147 waliopata maambukizi ya virusi vya Corona (COVID – 19) nchini, kati yao waliopona ni 11 na vifo 5 vimethibitishwa tangu kuanza kuripotiwa kwa ugonjwa huu nchini tarehe 16 Machi 2020. Wagonjwa wote waliobaki  (131) hali zao ni nzuri isipokuwa wanne (4) ambao wanapatiwa matibabu ya wagonjwa mahututi kutokana na kuwa wana wanasumbuliwa na matatizo mengine ya kiafya. Ripoti kamili isome HAPA

Loading