Wizara ya Afya yapokea msaada kutoka WHO kwa ajili ya chanjo kipindupindu Posted in News and Events By News Room On June 30, 2021July 1, 2021 Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Nassor Ahmed Mazrui (kulia) akipokea boksi la vifaa vya usajili kwa ajili ya chanjo ya kipindupindu inayotarajiwa kutolewa kuanzia Julai 3 hadi 7 katika shehia 56 ambazo huathirika na maradhi ya Kipindupindu mara kwa mara, huko Ofisini kwake Mnazimmoja Baadhi ya Vifaa walivyokabidhiwa Wizara ya Afya na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Andemichael Ghirmy kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma ya Chanjo ya Kipindupindu inayotarajiwa kutolewa kuanzia Julai 3 hadi Julai 7 katika shehia 56 ambazo huathirika na maradhi ya Kipindupindu mara kwa mara Nchini Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Andemichael Ghirmy (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusiana na vifaa mbalimbali alivyovikabidhi kwa Wizara ya Afya ikiwa ni msaada kwa ajili ya Chanjo ya kipindupindu, hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja