WIZARA YA AFYA YATILIANA SAINI MKATABA WA UIMARISHAJI WA MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA

Hafla hiyo ya utiaji saini ilifaywa na  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinisia na Watoto, Dk. Fatma Mrisho pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma kutoka Shirika la ABT Associates, Emmanuel Malangalila, katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya utiaji saini Mkurugenzi Emmanuel Malangalila alisema Mradi huo unakusudia kulenga kuboresha huduma bora kwa wananchi wanaoishi mazingira magumu.

Aidha alisema kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mradi huo pia una lengo la kuimarisha utawala bora ili kuongeza zaidi uwazi na uwajibikaji kwa wananchi katika ukusanyaji wa mapato na matumizi yake.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisema mradi huo  utaimarisha mfumo wa kuandaa mipango ya bajeti na mifumo ya uhasibu ili kutoa tarifa za fedha katika vituo vya  kutolea huduma na kupanga kukusanya matumizi bora ya rasilimali.

Sambamba na hayo, alisema mradi huo utaboresha kutumia mifumo ambayo itaweka mahusiano kwa ajili ya utawala bora ili kuhakikisha rasilimali zinakidhi mahitaji husuani kwa wanawake na vijana.

Nae  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Dk. Fatma Mrisho amelishukuru shirika hilo ambalo litasaidia  Serikali kuzidi kuimarisha huduma za afya Zanzibar.

Loading