ZIARA YA KUKAGUA HUDUMA ZA AFYA UWANJA WA NDEGE

 Afisa Dhamana huduma za afya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Nassor Hamadi Saidi akitowa maelezo kwa Naibu Mkurugenzi wa Idara ya kinga na Elimu ya Afya, kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinisia na Watoto,  Dk. Salim Slim katika ziara ya kukagua huduma za afya Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Afisa dhamana huduma za afya uwanja wa ndege  Nassor Hamad Said amesema hayo katika ziara iliyofanywa na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya ya Wizara ya afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto.

Amesema iwapo wasafiri watafanya maombi kwa njia ya mtandao itawezesha kupata majibu ya kipimo ya uviko 19  mapema kupunguza  foleni wakati wa safari  na msafiri kuondoka kwa wakati .

Aidha alifahamisha ni vyema wasafiri wakawasiliana na mashirka yao ndege mapema na wakala wao wanaosafirisha kufanya maombi yao kwa njia ya mtandao ili kupunguza foleni.

Amesema mbali ya changamoto hiyo pia wanakabiliwa na uchache wa vitendea kazi pamoja na uhaba wa wafanyakazi na kupelekea kutofanya kazi kwa ufanisi uanaotakiwa

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Salim Slim  amesema changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa  Kitengo cha afya Uwanja wa ndege Zanzibar  watazifanyia kazi kwa haraka ili waweze kutoa huduma bora kwa wasafiri

Amesema wafanyakazi wa kitengo hicho wanafanya kazi kubwa ya kuwahudumia wasafiri wanaotoka na  wanaongia nchini hivyo watahakikisha huduma zinazotolewa kwa wasafiri zinakuwa ubora wa hali ya juu.

Alifahamisha kuwa   kitengo hicho kinahitaji  kuwa na wafanyakazi wa kutosha sambamba na vitendea kazi pamoja na kuimarisha mifumo ya kutoa huduma za kupima  uviko 19 kwa wasafiri wanaotoka na wanaongia nchini.

Vilevile alifahamisha kuwa watahakikisha kuwa wanaimarisha mifumo ya upimaji wa uviko 19 ili wasafiri wapate huduma mara moja na kuondoka kwa wakati uliopangwa.

Loading