KITENGO CHA LISHE WIZARA YA AFYA ZANZIBAR CHAWATAKA WANAHABARI NA WALIMU WA MADRASA KUSAIDIA KUHAMASISHA JAMII

Afisa Lishe Kitengo cha Lishe Wizara ya Afya Subira Bakari Ame akitoa takwimu za utoaji  wa Vitamin A kwa watoto na dawa za minyoo pamoja na mikakati ya kuboresha zoezi la mwezi wa sita katika Mkutano uliofanyika Kitengo Shirikishi cha mama na mtoto Kidongochekundu.

Wilaya ya Kaskazini B imetajwa kuwa Wilaya iliyo chini zaidi katika kutekeleza zoezi la kuwapatia Watoto wao Vitamin A na Dawa za Minyoo hivyo juhudi zinahitajika zaidi kuondosha tatizo hilo.

Afisa Lishe Kitengo cha Lishe wa Subira Bakari Ame amebainisha hayo wakati akitoa takwimu za zoezi lililofanyika Mwezi Disemba mwaka jana kwa Waandishi wa habari na Wadau wengine wa afya katika ukumbi wa Hospital ya Wagonjwa wa akili Kidongo chekundu.

Amesema hali hiyo inatokana na sababu mbali mbali ikiwemo uelewa mdogo wa elimu ya afya na ushirikiano hafifu wanaoupata kutoka kwa Wadau tofauti wa Wilaya hiyo.

Hivyo amesema ipo haja kufanyika kwa mjadala wa pamoja kubaini chanzo cha tatizo ili kuifanya Wilaya hiyo kufikia viwango sawa na Wilaya nyingine.

Kwa upande wao washiriki wa Mkutano huo walipedekeza kutengenezwe Bajeti maalum ya kuongeza elimu ya Afya kwa Wilaya hiyo.

Aidha wamesema ipo haja ya kuishirikisha jamii yote ikiwemo Wazee na Walimu wa Madrsa badala ya kuwaachia Masheha na Wajumbe wao kusimamia zoezi la kuhamasisha jamii kutekeleza zoezi hilo.

Loading