WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA UJUMBE WA UN

Mwakilishi Mkaazi Wa Shirika La Afya Duniani (Who) Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay akiukaribisha ujumbewa wa UN kwa Waziri wa Afya Zanzibar walipofika Ofisini kwake pamoja na kutoa maelezo kuhusu juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha huduma za Afya Zanzibar.

Mashirika ya kimataifa un, who na unicef yameeleza kuridhishwa na huduma bora za afya zinazotolewa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar hali iliyopelekea kuwa nchi ya mwanzo miongoni mwa nchi 11 kupelekewa mradi wa majaribio wa kuimarisha huduma bora za afya.

Akizungumza na waziri wa afya hamad rashid mohamed ofisini kwake, mkuu wa sekreteriate ya mtandao wa kutoa huduma bora za afya wa who kutoka makao makuu geneva blerta maligi amesema katika mradi huo watazingatia maeneo yaliyo na upungufu ili kuyaimarisha katika kufikia kutoa huduma bora zaidi za afya.

Amesema zanzibar ipo katika nafasi nzuri kutokana na kuimarika kwa huduma za afya ya msingi kuanzia ngazi ya vijiji hasa huduma za mama na mtoto.

Aidha amesisitiza suala la kuimarishwa mtandao wa pamoja katika taasisi na nchi mbali mbali ili kukuza utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

Bi. Maligi amesema kuwepo kwa huduma bora za afya ni pamoja na kuwa na madktari bingwa, wauguzi na vifaa tiba vya kutosha ili wananchi wengi wapate huduma kwa ufanisi.

Waziri wa afya mhe. Hamad rashid mohamed ameuhakikishia ujumbe huo kwamba suala la kuimarisha huduma bora za afya ni moja katika vipaumbele vya serikali ya mapinduzi ya zanzibar.

Alisema serikali inaendelea kutoa umuhimu mkubwa suala la kuwaendeleza kielimu madaktari na watendaji wengine wa kada nyengine za sekta ya afya na kuongeza vifaa tiba katika hospitali za mijini na vijijini.

Aliueleza ujumbe huo kwamba haukufanya makosa kuanzisha mradi wa majaribio wa kuimarisha huduma za afya zanzibar kutokana na hatua kubwa iliyofikiwa ya kutoa huduma bora za afya.

Alisema huduma za mama na mtoto zimeimarishwa na zinapatikana katika vituo vingi vya afya vijijini na hakuna ulazima kwa wananchi kufuata huduma hiyo katika hospitali kuu za mjini.

Ujumbe huo ulikuja zanzibar kwa mara ya kwanza kufanya utafiti juu ya utoaji wa huduma za afya na kugundua kubwa zanzibar iko vizuri katika huduma bora za afya ikilinganishwa na nchi nyingi za afrika.      Mwisho

 

Loading