UMOJA WA NCHI ZA ULAYA NDANI YA ZANZIBAR

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuwapatia chanjo ya Covid 19 wafanyakazi wa sekta ya Utalii ili kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa amani na usalama

Waziri Mazrui ameyasema hayo huko Ofisini kwake Mnazi Mmoja wakati alipotembewa na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya Mnafredo Fanti pamoja na Ujumbe wake kwa ajili ya kujitambulisha amesema sekta ya utalii ni sekta muhimu nchini katika kukuza uchumi ni vyema wafanyakazi wake wakapata kinga ya kujikinga afya zao dhidi ya maambukizi ya Corona na kufanyakazi kwa imani.

Amesema serikali itaanza na sekta hiyo kutokana na wafanyakazi wake kukutana na mchangamyiko wa watu mbalimbali na kuthibisha usalama wa wageni wanapoingia kwa watendaji wake

“Tunaanza kwa wafanyakazi hao kuapatiwa Chanjo ili kuzithibitishia nchi zinzoleta Watalii kuwa Zanzibar ni nchi  salama kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiutatalii”, alieleza Waziri huyo

Amefahamisha kuwa  watakaopatiwa chanjo hiyo ni pamoja na wafanyakazi wa hoteli, watendaji wa Viwanja vya Ndege, waongozaji watalii ili kufanyakazi kwa ufanisi na usalama.

Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fant amesema ana matumaini makubwa na  ameahidi kushirikianana na Zanzibar  katika kupambanana ugonjwa wa Covid-19 ambao ni janga lililoikumba Dunia nzima.

Hata hivyo amesema kuwa Umoja huo utakuza  mashirikiano zaidi ya kuisaidia Zanzibar katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo Afya, Kijamii, na kiuchumi.

Loading