CHAMA CHA WATAALAMU WA TIBA KWA VITENDO TANZANZIA YAHAMASISHA UTOAJI HUDUMA KWA VITENDO KWA WATU WENYE ULEMAVU WA VIUNGO ZANZIBAR

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akiwahutubia wazazi na Wataalamu wa tiba kwa vitendo Tanzania katika hafla ya ufunguzi wa Mkuutano Mkuu wa chama cha Wataalamu wa Tiba kwa vitendo Tanzania uliofanyaka Hospitali kuu ya Mnazimmoja Zanzibar.

Zaidi ya asilimia 60 ya watu wenye ulemavu Zanzibar wanaishi katika mazingira magumu kutokana na ukosefu wa ajira na kufanyiwa vitendo vya unyanyapaa katika jamii.

Hayo ameyasema Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wataalamu wa Tiba kwa Vitendo Tanzania huko Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.

Amesema watu wenye ulemavu wanaishi katika mazingira magumu kutokana na hali zao pamoja na kukosa huduma muhimu katika kujikimu kimaisha jambo ambalo hupelekea kufanyiwa vitendo viovu vya udhalilishaji.

Ameeleza kuwa kiwango hicho ni kikubwa kutokana na uelewa mdogo kwa jamii wa kuzitambua haki za watu wenye ulemavu ili waweze kutunzwa, kuthaminiwa na kupatiwa mambo ya msingi.

Waziri Hamadi amefahamisha kuwa lengo la chama hicho nikuwasaidia na kuwawezesha  watu wenye ulemavu kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii na kupata huduma za msingi kama walivyo watu wengine.

Waziri Hamadi ametembelea kitengo cha watu wenye ulemavu wa viungo katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja na kupata maelezo mbali mbali kutoka kwa Wataalamu wanaoshuhulika na tiba hiyo.

Rais wa Chama Cha Wataalamu wa Tiba kwa Vitendo Tanzania Godfrey S. Kimathy akisoma risala katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wataalamu wa Tiba kwa vitendo Tanzania huko Hospitali kuu ya Mnazimmoja.

Nae Rais wa Chama Cha Wataalamu wa Tiba kwa Vitendo Tanzania Godfrey S. Kimathy katika risala yake amesema lengo la Chama hicho ni kusimamia na kuratibu shuhuli zote kwa vitendo kwa watu wenye ulemavu wa viungo pamoja na kuwasaidia.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Ali Salim  amesema kitengo hicho kinakabiliwa na tatizo la uhaba wa vifaa na kupelekea kukosekana kwa baadhi ya huduma na uhaba wa wataalamu katika sehemu hiyo.

Loading