WAZIRI UCHUMI WA BULUU AFUNGUA KONGAMANO SIKU 16 ZA HARAKATI ZA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI NA UDHALILISHAJI

Waziri wa Uchumi wa Buluu Abdalla Hussein Kombo akifungua kongamano la Vijana la kuadhimisha siku 16 za harakati za kupinga Ukatili na udhalilishaji wa kijinsia katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni mjini Zanzibar.

Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi Abdalla Hussein Kombo, ameitaka jamii kushirikiana kwa pamoja katika kuondosha vitendo vya udhalilishaji nchini, kwani vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku.

 Ameeleza hayo huko ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni wakati  akifungua Kongamano  la vijana la kuadhimisha siku 16 za harakati za kupinga vitendo vya UIkatili na Udhalilishaji.

Amesema   wazazi,walezi pamoja na walimu wa skuli na madrasa wanajukumu la  kusimamia vyema malezi ya watoto kwa kuwalea katika malezi yenye maadili mema ili waweze kuepukana na vitendo viovu vya uhalilishaji.

Aidha  amewataka vijana kuachana na tabia ya kukaa vijiweni, jambo linapelekea ushawishi wa kufanya vitendo visivyofaa kwa jamii, na badala yake wajiunge na vikundi vya ujasiriamali ili waweze kujipatia mahitaji yao ya lazima.

Pia ameeleza kuwa vijana wengi wamekuwa wakijishughulisha sana na mitandao kwa kuperuzi na kuangalia picha za ngono sambamba na mambo ya wasinii ambayo  yanapotiosha utamaduni wetu ikiwemo mavazi .

Nae Mkurugenzi wa Elimu Mbadala na Watuwazima, Mashavu Ahmada Fakih,ameiambia jamii kuwa wazazi hawapaswi kuwafungisha ndoa watoto wakiwa katika masomo jambo ambalo hupelekea kupoteza malengo yao ya baadae.

Alieleza kuwa hivi karibuni wamesitisha ndoa za wanafunzi  5 ambao bado wanaendelea na masomo yao.

Vile vile amewataka wanafunzi kujitambua wanapokua mashuleni na kuwa makini na masomo yao ili waweza kufikia malengo waliyojiwekea   hapo baadae.

Vilevile amewashauri wanafunzi  kujishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile computure, ufundi na hata biashara mara tu wamalizapo masomo yao ili wajipatie kipato cha halali na kuepukana na suala zima la udhalilishaji.

Akitoa takwimu ya Vitendo vya udhalilishaji kutoka mwezi  Januari hadi Novemba mwaka huu, amesema Wilaya ya Magharibi “A” inaongoza kuliko wilaya zote kwa kuwa na kesi 260 ikifutiwa na wilaya ya Magharibi “B” ambayo ina jumla yua kesi 243 .

Kongamano hilo lilojumuisha Vijana na Wadau mbali mbali wa kupinga Vitendo vya ukatili na Udhalilishaji lilibeba ujumbe usemao “tuimarishe amani Zanzibar,tumalize vitendo vya ukatili na udhalilishaji sasa ”.

Loading