WAZIRI WA AFYA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA NA BINGUNI

Waziri wa Afya alifanya  ziara ya  kutembelea baadhi ya vitengo vya Hospitali kuu ya Mnazimmoja na kupata fursa ya kuzungumza na wagonjwa na kujionea changamoto zilizopo hospitalini  hapo.Akitaja changamoto zinazowakabili katika Hospitali hiyo Mkurugenzi Mtendaji  Dkt Msafiri Marijani amesema kuwa kuna baadhi ya vitengo kuna upungufu wa wafanyakazi vitendea kazi  pamoja na upungufu wa baadhi ya dawa hasa kwa wenye matatizo ya Saratani. Aidha alipata nafasi ya kutembelea Wodi Mifupa, Wodi ya Wazazi, Wodi ya Watoto, Theater,Maabara na  Wodi waliopata ajali.Pia Waziri huyo alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni na kujionea hali halisi ya ujenzi huo na sababu zilizopelekea kusimama kwa ujenzi huo.Akitaja sababu za kusimama kwa ujenzi huo Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya utafiti wa Afya Dr. Mayasa Salum Ali amesema ni pamoja na ukosefu wa fedha na baadhi ya vitendea kazi ikwemo usafiri na mkonga wa intaneti ambao utawarahishia ufanyaji wa kazi zao.

Loading