Timu ya Madaktari kutoka CUBA na Zanzibar waliowasilisha tafiti mbali mbali za maradhi wakiwa na Viongozi wa Serikali ya Zanzibar (aliyekaa katikati ) , Waziri wa Afya Hamad Rashid( kushoto) Waziri wa Elimu Riziki Pembe Juma na Balozi wa CUBA Profesa Lucas Domingo huko Skuli ya Afya Mbweni Zanzibar
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed imesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarisha mashirikiano na nchi mbali mbali ili kuwapatia huduma za matibabu wananchi wa Zanzibar
Hayo ameyasema leo huko katika Skuli ya Afya Mbweni wakati wa Mkutano wa Madaktari wa Cuba na Zanzibar wakati walipowasilisha Tafiti zao za maradhi mbali mbali waliyoyafanyia uchunguzi ambayo yameonekana kushamiri duniani kote na kupatiwa huduma za matibabu.
Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania na Serikali ya Zanzibar ina mashirikiano makubwa na Serikali ya Cuba na ya muda mrefu kwa lengo la kuboresha huduma za tiba kwa maradhi sugu ambayo yanaikabili jamii.

Aidha alisema kuwa tafiti zinajionyesha ugunduzi wa tiba utasaidia wagonjwa kurudia katika hali zao za kawaida pamoja na kuepukana na ulemavu usiotarajiwa hasa kwa wale wagonjwa wa sukari.
Alieleza kuongezaka kwa wataaluma nchini kutoka katika nchi tofauti kutasaidia mashirikiano ya kimatibabu na kuengeza ujuzi kwa Madaktari Wazalendo jambo ambalo litasaidia kuimarisha huduma za kimatibabu nchini.
Nae Mkuu wa Skuli ya Afya Suza Salum Seif Salum akielezea utafiti kuhusu kudhibiti mazalia ya mbu alisema kuwa ongezeko kubwa la mazalio ya mbu linatokana na uchafu wa mazingira katika maeneo mbali mbali ya mji hasa katika baadhi ya mitaa ambayo hutuwama maji na kusababisha mazalio ya mbui maeneo ambayo yameonyesha kuwepo na mazalio mengi ni kikwajuni juu na bondeni
” Wizara ya Afya kwenye kitengo chetu cha kuondosha maradhi kinachukua juhudi za kuwaangamiza mbu hao ambao husababisha maradhi ya Malaria, homa ya manjano na pia homa ya kinyungu’nya na kuhakikisha wanapotea kabisa.”,alisema DK,Salum.

Kwa upande wa Msaidizi wa Skuli ya Afya Mbweni Amina Abdulkadir Ali wakati akiwasilisha mada ya uuguzi na wakunga alisema inapaswa wauguzi kuzingatia mambo matatu muhimu katia kutoa matibabu kwa wagonjwa kwanza kichwa mikono na moyo ,kwa kuweza kuwa na moyo wa huruma na kutumia lugha nzuri wakati wa kuhudumia wagonjwa .
hata hivyo alisema kada ya uuguzi na ukunga imeweza kutimiza miaka 200 kwa sasa hivyo wataitumia kuisherehekea kwa kutoa elimu kwa wauguzi na wakunga wa kila Wilaya ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Mada zilowasilishwa ambazo zimefanyiwa utafiti na Madaktari kutoka Cuba ni pamoja na kensa ya kizazi, ziwa ,kisukari na maradhi mengine yaliyo sugu kupatiwa uvumbuzi.
Mkutano wa Timu ya Madaktari kutoka CUBA ni wa mara ya tatu kufanyika Zanzibar kwa lengo la kubadilishana utaalamu wa kimatibabu.