ZANZIBAR YAANDAA ENEO LA KUWAWEKA WAGONJWA WA CARONA PINDI WAKITOKEA

Mganga Mkuu wa Serekali ya Tanzania bara Prof. Muhammed Bakari Kambi akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mashirikiano na wenzao wa Zanzibar juu ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona pindi ukingia nchini.

Ujumbe wa Wataalamu wa Afya kutoka Tanzania Bara na Zanzibar Umetembelea jengo la dharura  lililotengwa kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa watakaogundulika na viashiria vya ugonjwa wa Corona liliopo Kidimni Wilaya ya Kati Unguja.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid Salum wakati walipotembelea Jengo hilo kwa ajili kulikagua na kujua maendeleo yake, amesema Serikali imeamua kufanya maandalizi hayo kutokana na ugonjwa huo tayari yameshaingia Afrika kufuatilia muingiliano wa wageni.

“Eneo hili ni maalum lililotengwa kwa kuwahifadhia wagonjwa wataogundulika na ugonjwa huo hatarishi ambao huambukiza kwa njia ya hewa na kusambaa kwa haraka sana kwa kuweza kuudhiti usienee”, alieleza.

Ameeleza kuwa kwa sasa hakuna mtu yoyote aliyegundulika na viashiria vya maradhi hayo, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari kwa ajili ya kuweza kuudhibiti ugonjwa huo.

Nae Mganga Mkuu kutoka Tanzania Bara Profesa Mohamed Bakari amesema watashirikiana na Serikali ya Zanzibar katika kutoa huduma na kuudhibiti ugonjwa huo.

Amefahamisha kuwa  ni lazima kujipanga  mapema katika kukabiliana na ugonjwa huo kwani maradhi ya corona yanasambaa kwa haraka kutoka kwa mtu mmoja  kwenda kwa mwengine hivyo ni vyema kuchukua tahadhari kwa kutenga maeneo ya kawahifadhi watakaoathirika na ugonjwa huo

Profesa Mohamed ameeleza kuwa serikali zote mbili zimeweka vifaa maalum vya kuwatambua wageni wanaoingia nchini.

Hata hivyo aliwatoa hofu wananchi  kwa kusema Tanzania hadi sasa ipo salama na wageni wote wanao ingia wanakaguliwa ili kulinda hali za wananchi wao.

Ujumbe huo ulikagua Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Aman Karume, Bandari ya Zanzibar Malindi pamoja na Jengo  la Kurekebisha Tabia (Soba Hause) liliopo Kidimni

Loading