ZIARA YA KAMATI YA USTAWI WA JAMII YA BARAZA LA WAWAKILISHI

Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya  Baraza la Wawakilishi Mwanaasha Khamiss Juma akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya Ziara yao ya kuangalia  maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya Wagonjwa watakaogundulika na Virusi vya Corona (kulia) ni Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed.

Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid amewataka wananchi kuondoa  hofu  juu ya uvumi uliopo kuhusiana ugonjwa wa Corona kuingia nchini.

Waziri Hamad amesema kufuatia kuwepo kwa washukiwa wawili raia wa Ujerumani waliofika katika hospitali ya Global kwa ajili ya kupata matibabu ambao bado hawajathibitka kuwa na ugonjwa huo.

Alisema kuwa maradhi hayo bado hayajathibitika Zanzibar wananchi wasiwe na wasiwasi kutokana na ugonjwa huo kwani serikali itatoa taarifa kamili na haitoficha jambo lolote kuhusu janga hilo.

Amesema Serikali iko makini tayari imeshaweka mandalizi ya kutosha ili kudhibiti ugonjwa huo,

“Serikali iko makini na tayari imeweka maandalizi ya kutosha ili kudhibiti ugonjwa huo, lolote litakalotea serikali itatoa tamko” alieleza Waziri Hamad.

Wakati huo huo kamati ya Ustaw wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi ilifanya ziara ya kutembelea Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Bandarini pamoja na Kituo cha dharura cha matibabu ya ugonjwa wa Corona Kidimni kuona jinsi vituo hivyo  vilivyojipanga kudhibiti Virusi vya ugonjwa huo visingie nchini.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwanaasha Khamis Haji amesema kamati imeridhishwa na maandilizi yaliyofanywa na serikali kutokana na kuwepo kwa vifaa vinatakavvohitajika kutoa huduma katika vituo hivyo.

Aidha ameutaka uongozi wa Bandari na Mamalaka ya Viwanja vya Ndege kutoa ushirikiano na Wizara ya afya ili kuweza kuzuia na kudhiditi ugonjwa huo nchini.

Kwa upande wake Msaidizi Mkuu wa Kituo cha Afya Uwanja wa Ndege Mohamed Khamis Ali amesema Mamlaka imeweka utaratibu maalum kwa wageni wanaoingia nchini, kuwapima kwa kutumia vifaa maalum ili kuweza kutambua afya zao.

“Tumeweka utaratibu maalumu kwa wageni wanaoingia nchini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anavua vidhibiti vya ugonjwa huo alivyotumia safarini ikiwemo glaves na maski,kunawa mikono kwa dawa maalumu na kupimwa kwa kutumia mashine malumu ya kuweza kutambua ugonjwa huo”. Alifahamisha Msaidizi huyo.

Loading