Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed na Balozi wa Cuba Professor Lucas Domingo Hernandez wamesaini Mkataba wa uimarishaji huduma za afya kwa wananchi wa Zanzibar, Hafla hiyo imefanyika huko Ofisini kwake Wizara ya Afya Mnazimmoja
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Cuba imetiliana saini mkataba wa uimarishaji wa huduma za Afya kwa lengo la kuwasaidia wananchi wanaosumbuliwa na maradhi mbali mbali hasa ya sukari ambayo yatapatiwa chanjo maalumu ya ukaushaji vidonda
Hafla hiyo ya utiaji saini umefanyika huko Ofisini kwake wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja baina ya Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed na Balozi wa Cuba Professor Lucas Domingo Hernandez mkataba ambao una lengo la kuimarisha afya kwa wananchi wa Zanzibar.
Waziri Hamad amesema Cuba wana mashirikiano makubwa katika masuala ya kuboresha mambo mengi ya maendeleo ikiwemo Afya, elimu na Kilimo.
Amesema Nchi ya Cuba inongoza katika mambo mbali mbali ya afya na pia madaktari wa Zanzibar wanapatiwa mafunzo ya kutoa huduma kwa wagonjwa yenye lengo la kuimarisha ujuzi zaidi wa kimatibabu nchini.
Aidha amesema mafanikio mengi yamepatikana kutoka nchini huko ikiwemo kuwaleta madaktari bingwa kuja kuwatibu wagonjwa na kutoa elimu ya kitaalamu kwa madaktari wa Zanzibar ambapo nchi yao inaongoza kwa kutoa huduma ikiwemo matibabu.

Nae Balozi wa Cuba profesa Lucas Domingo amesema hivi sasa wamevumbua dawa inayoitwa HEBER PROT –P ambayo inakausha vidonda vya sukari na kuwaondoshea wagonjwa wa maradhi hayo kukatwa miguu au viungo vyengine.
Amesema baada ya kuonekana wagonjwa wengi wa sukari wanapopata vidonda Zanzibar na kushindikana kutibika hadi kupelekea kukatwa miguu au baadhi ya viungo vyengine hivyo dawa hiyo itasaidia kuondosha na badala yake inapelekea kukauka kwa vidonda hivyo .