Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed wakati alipofanya ziara ya kuangalia Ujenzi wa Maabara ya Uchunguzi na Utafiti wa Virusi katika Eneo la Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.