WAANDISHI WA HABARI WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU CHANJO YA KIPINDUPINDU DOZI YA PILI

Msimamizi wa Chanjo ya Kipindupindu Unguja Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla amesema chanjo ya kipindupindu haina mahusiano na chanjo ya corona 19 na wala haina madhara yoyote kwa binadamu. Hayo ameyasema huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo  wakati alipokuwa akitoa  mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu Umuhimu wa kumaliza Dozi ya Pili ya chanjo hiyo Amesema chanjo  […]

KATIBU MKUU MPYA AKABIDHIWA RASMI OFISI

Waziri wa Afya ,Ustawi wa Jamii, Wazee ,Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui amewataka watendaji wa wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya awamu ya nane. Hayo aliyasema katika hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Katibu Mkuu yaliyofanyika Wizarani  hapo mara baada ya kuapishwa kwa Katibu Mkuu mpya waWizara hiyo Alisema […]

WAZIRI WA AFYA AFUNGUA KONGAMANO LA KUTATHIMINI KAZI ZA WAKUNGA NA WAUGUZI ZANZIBAR

Wauguzi na Wakunga Nchini wametakiwa kufata maadili na sheria za kazi katika kutekeleza majukumu yao ili kutoa huduma bora kwa  wazazi na wananchi wa Zanzibar. Akizungumza mbele ya wauguzi na wakunga katika kongamano la kutathmini kazi za Uuguzi na Ukunga Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil,  Kikwajuni Mjini Unguja, Waziri wa Afya,Ustawi […]

UMOJA WA NCHI ZA ULAYA NDANI YA ZANZIBAR

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuwapatia chanjo ya Covid 19 wafanyakazi wa sekta ya Utalii ili kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa amani na usalama Waziri Mazrui ameyasema hayo huko Ofisini kwake Mnazi Mmoja wakati alipotembewa na Balozi wa Umoja wa […]

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA UZINDUZI WA KAMPENI YA UGAWAJI VYANDARUA KITAIFA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na Wafadhili mbalimbali katika kupiga vita dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini. Hayo aliyasema Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui,  wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa Vyandaruwa uliofanyika Kitaifa Katika Uwanja wa Demokrasia , Kibandamaiti . Alisema kutokana […]

Loading